Ama hakika sasa dunia sasa ni kijiji, na inatubidi sana kuangalia
matendo yetu na picha unazozipost katika mitandao ya kijamii, maana
inasambaa kama moto unaoteketeza pori. juzi nilikuwa nikipokea na kuona
picha ya askari wawili wa usalama barabarani wakiwa katika hali ya
kimapenzi, picha ikiwaonyesha wakiwa wana-kiss huku wakiwa kazini na
sare za kazi.
Imeaminika kuwa wawili hao ni Trafick kutoka mkoa wa Kagera, na kwa
taarifa zilizopo sasa ni kuwa tayari Jeshi la Polisi Kagera limechukua
uamuzi wa kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na askari aliepiga
picha hii kupitia simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni
PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhili Linga mwenye
namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa
kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
Kamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na
kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha
kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC
Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya
mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho
ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni
picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua
maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya
kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.
chanzo: DJ FETY BLOG
0 comments:
Post a Comment