Waziri
Wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa amewataka Wakaguzi wa Shule
kuhakikisha ripoti zitoa kwa wamiliki wa shule, shule, bodi za shule na kwa
walimu baada ya ukaguzi shuleni
zinafanyiwa kazi mara moja ili kupunguza changamoto zinazoikabili sekta
ya Elimu.
Mhe.
Dkt Kawambwa aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika uzinduzi
wa maadhimisho ya Wiki ya Ukaguzi kitaifa iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE)..
“Wamiliki wa shule mnapaswa kufanyia kazi
ripoti zinazotolewa na Wakaguzi wa Shule badala ya kuziweka katika makabati, lazima tuhakikishe mapungufu yote yaliyobainishwa yanapatiwa
ufumbuzi mara moja ili kuninua ubora wa Elimu.” Alisema Dkt. Kawambwa.
Aidha,
amesema ni aibu kwa Wakaguzi wa Shule kuendelea kukagua na kukutana na changamoto
zilezile ambazo walikutana nazo wakati walipofanya ukaguzi kwa mara ya kwanza
na kuzitolea ripoti kwa wamiliki wa shule na bado hazifanyiwi kazi..
Hata
hivyo Dkt. Kawambwa, aliwambia wadau wa
Elimu kuwa zipo changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya Elimu, ambazo ni
pamoja na uhaba wa rasilimali watu, rasilimali fedha, utendaji na usimamizi
mbovu, msongamano wa wanafunzi darasani, utoro, uhaba wa walimu wa masomo ya
sayansi na hisabati, uhaba wa Majengo,
na uhaba wa maabara.
Waziri
amesema changamoto nyingi katika sekta ya Elimu zinatokana na ukosefu wa
ushirikiano kati ya Wizara na wadau wa Elimu, na hivyo basi kuwaomba wazazi na jamii
kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja ili kuleta
mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu.
Dkt.
Kawambwa amewataka wananchi na wadau wa Elimu kuwauliza wakaguzi wa shule, ni
mara ngapi wamezikagua shule na wameshauri nini na je ushauri huo umezingatiwa
na kufanyiwa kazi, yote hayo yanahitajika ili kufanikisha Mpango mpya wa
Matokeo Makubwa Sasa (Bigi Results Now-BRN).
Waziri
akiitimisha hotuba yake katika kongamano hilo la wiki ya ukaguzi aliwasihi
wadau wa Elimu kuitumia vizuri kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema “Ukaguzi
Fanisi Na Endelevu Kwa Elimu Bora” kujadili kwa kina mada zote
katika kongamano hilo zitakazo wasilishwa na wataalamu ili kupata
matokeo yanayotarajiwa katika sekta ya Elimu nchini.
0 comments:
Post a Comment