Sunday, 27 July 2014

HABARI YA ISRAEL & PARESTINA MAPIGANO


 
Leo tar 27/07/2014
Jeshi la Israel limesema kuwa linaendeleza mashambulizi yake katika eneo la Gaza .
Hatua hiyo inajiri baada ya wapiganaji wa Kipalestina Hamas kurusha takriban makombora 20 nchini Israel licha ya makubaliano ya kusitisha vita kuongezwa kwa masaa mengine 12 kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa.
Kundi la Hamas limesema kuwa halitasita kutekeleza mashambulizi hadi wanajeshi wa Israel watakapoondoka ndani ya maeneo ya Palestina.
Mwanajeshi mmoja wa Israel anadaiwa kuuawa na shambulizi la roketi usiku kucha.
Siku ya jumamosi raia wengi wa Gaza walitumia fursa ya kusitishwa kwa vita hivyo kutembelea maeneo mengi yalioharibiwa karibu na mpaka na Israel huku miili ya raia wa Palestina waliouawa ikiendelea kufukuliwa kutoka kwa vifusi vya majengo yalioharibiwa.
Source BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment